Lijualikali Aupasua Upinzani Mbele Ya JPM “Tulikuwa Tunakutana Na Wazungu Wamegeuka”Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kilombero (CHADEMA) Peter Lijualikali amesema vingozi wa vyama vya upinzani nchini walikuwa wanafanya vikao na wazungu kujadili mustakabari wa nchini.

Akizungumza baada ya kupewa nafasi ya kusalimia wananchi na Rais John Magufuli wakati akihutubia wananchi wakati wa kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa mahandaki ya reli.

“Watu wanakulalamikia kwa sababu wana mipango yao, sisi upinzani tukikuwa tunaenda kuwaona hao wazungu walikuwa wanatuambia demokrasi sio muhimu kuliko amani lakini sasa hivi unavyogusa maisha yetu wananchi wa chini wamegeuka wanasema demokrasia ni muhimu” amesema Lijualikali.

Ikumbukwe kuwa Peter Lijualikali aliomba kuhamia kwenye chama cha Mapinduzi (CCM) bungeni baada ya kufukuzwa na chama chake cha awali Chadema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments