6/25/2020

Manara Aanza Mbwembwe Upya Simba


OFISA Habari wa Simba, Haji Manara, amerudia kauli yake kuwa Simba itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara 10 mfululizo, baada ya juzi kutandaza soka la kitabuni na kuishushia Mwadui kichapo cha mabao 3-0 Uwanja wa Taifa, Dar.

Manara alisema kuwa mpango mkubwa uliopo ndani ya klabu hiyo ni kuona kwamba wanaendeleza hesabu pale walipoishia msimu uliopita.

“Tunatarajia kutwaa mataji 10 ya Ligi Kuu Bara mfululizo ili kuongeza heshima na ukubwa wa Simba ambayo ipo vizuri na imejipanga katika kila kitu ukianzia wachezaji mpaka benchi la ufundi.

“Kuna mataji mawili ambayo tumeyachukua mfululizo, hivyo msimu huu tunasaka taji la tatu na tukishawasha gia yetu hatushikiki, ni mwendo wa ‘back to back’ kwenye ligi,” alisema.

Simba ilitwaa ubingwa mara mbili mfululizo ambapo ilianza msimu wa 2017/18 na 2018/19, kwa sasa inasaka kubeba taji la ligi mara ya tatu kwa msimu wa 2019/20, ipo nafasi ya kwanza na pointi zake 75
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger