Mondi Amponza Husna Maulid, Kupenda Ni Gharama!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Kupenda wakati mwingine ni gharama! Kitendo cha kuonesha upendo wake kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kimemtokea puani Mshiriki wa Miss Tanzania 2011, Husna Maulid, Amani linakumegea mchapo kamili.

 

Iko hivi; kupitia ukurasa wake wa Instagram, siku za hivi karibuni mrembo huyo alionekana kumposti mara kwa mara Diamond au Mondi na kusindikiza na jumbe mbalimbali.

 

Kuna ambayo alimweka Mondi akiwa ametinga miwani meusi na kitambaa cha njano kichwani kisha akaandika neno moja tu; ‘lion’.



Kama hiyo, haitoshi kuna nyingine alimposti staa huyo anayetamba na wimbo wa Jeje akiwa na kitambaa cheusi na kuandika; ‘Nasibu kama Nasibu’.

Juzikati kwenye Sikukuu ya Wababa, mrembo huyo alikwenda mbali zaidi kwa kumtupia Mondi akiwa ametinga kitambaa cheupe kichwani na kusindikiza na ujumbe uliosomeka; ‘Happy Father’s Day’.



AAMBULIA MATUSI

Tofauti na matamanio yake ya kuonesha upendo, kwenye picha hizo Husna ‘alioga’ matusi kama yote kutoka kwa mashabiki wanaomfuata kwenye ukurasa wake.Mashabiki hao walimwambia anajipendekeza kwa Mondi, hana lolote atafute mahali pa kutokea na si kwa Mondi ambaye hawezi kuwa na mpango naye hata kidogo.“Unapenda kumposti mtu ambaye hajawahi hata kukuposti, unajikutaga Zari au Tanasha?”“Hawezi kutoka na wewe takataka, endelea kujipende keza.”“Ovyoooooo.”“Shoobo tu fyuuu.” Hayo ni baadhi ya maoni ambayo yalikuwa yana afadhali kuandikika gazetini, mengine yalikuwa ni matusi mazito yasiyofaa kuchorwa gazetini.

AHUSISHWA NA ZARI

Kwenye baadhi ya page za udaku, kuna ambao walieleza kuwa penzi la Husna na Mondi lipo kweli na tayari habari zimeshamfikia Zari ambaye ameshaanza kurusha mashambulizi kwa Husna.

Kama hiyo haitoshi, page hizo zimeenda mbele zaidi kwa kusema kuwa mrembo huyo amepangiwa nyumba na Mondi na ndicho kilichomuongezea hasira Zari.

 

“Sijui itakuwaje maana nasikia bibie (Husna) kapangiwa nyumba na hivi tunavyoongea juzi kamposti Mondi kwenye siku ya wababa, inaonesha yule mtoto aliojifungua hivi karibuni, inawezekana ni wa Mondi,” mdaku mmoja aliandika huko Instagram.

AMANI LAMSAKA HUSNA

Amani lilimvutia waya mrembo huyo na kumsomea mashtaka yake ambapo aliyapangua moja baada ya lingine.Kuhusu suala la Zari kushtukia posti zake kwa Mondi, Husna alisema:“Yeye si kashaachika, anataka nini tena? Mwanaume ndio unatakiwa akung’ang’anie sio wewe umng’ang’anie.

 

Ninaona posti zake anazoandika kuhusu mimi lakini sitaki kumjibu,” alisema Husna na kuongeza: “Kama wewe ni mwanamke unayejiamini, huwezi kutukana eti kisa mwanaume.”Alipoulizwa kuhusu kutembea na Mondi au la, Husna aliishia kucheka na kusema:“Mimi siwezi kusema chochote, mambo yote yanaonekana kwenye mitandao.”Alipoulizwa kuhusu kupangiwa nyumba na Mondi, Husna alisema:“No comment.”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad