6/21/2020

Mwanamuziki Malaika Afunguka "Sina Wivu na Zuchu"MWANA-MUZIKIkutoka Bongo Flevani aliyetamba na ngoma kama Zogo, Sare na nyingine, Diana Exavery ‘Malaika’ amesema hana wivu wala kinyongo kwa wanamuziki wenziye wa kike wanaotamba kwa sasa kama Zuchu.Amesema kila mtu ana kipaji chake na ni vizuri kukubali kitu anachofanya mwenzako.

Malaika pamoja na kwamba hajaachia ngoma mpya kwa muda mrefu, lakini siyo sababu ya yeye kutozikubali ngoma za wenzake.

“Sina wivu wala kinyongo kwa wanamuziki wenzangu wa kike kama Zuchu kwa sababu wamethubutu mno na kwa sasa wanafanya vizuri sana. Mimi ni shabiki wao namba moja kwa sababu kila jambo na wakati wake,” amesema Malaika
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger