Niko Tayari Kuwa baby Mama wa Nne wa Diamond Amber Lulu Asema yuko Tayari Kumzalia DiamondStaa wa bongo Diamond Platnumz licha ya kuwa na baby mama watatu kuna wale wanamhitaji sana awe baba wa watoto wao na wanafanya chochote kile ili kuhakikisha wamempata.

Diamond anaweza kuwa na miaka 30, lakini amefanya mengi katika miaka yake kuliko vile wengi wamefanya, pia ni miongoni mwa wasanii bora afrika mashariki na kufahamika sana na mashabki wake.

 Video ya vibao vyake kwenye youtube kwa hakika zimetazamwa na watu zaidi ya billioni moja, huku akiwa miongoni mwa wasanii wanaotazamwa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Amber Lulu amekuwa akimposti Diamond kwenye mitandao yake ya kijamii, huku akisema kuwa anampenda msanii huyo huku akiwa tayari kumzalia mtoto.


Lulu alizungumza haya akiwa kwenye mahojiano Dar Es Salaam, Lulu alisema kuwa anampenda Dangote kwa sababu mbili tu moja ni kuwa Simba hajawahi kata tamaa na sababu ya pili maumbile tu yake.

 “Nampenda Mondi (Diamond) kwa sababu ni fighter, hustler lakini pia mwangalie amekata body. Ukimwangalia, unachanganyikiwa

“Akisema ananiona nakubali na natulia kabisa. Sasa hivi najibrand nataka niwe kama Zari na Tanasha. Naenda gym nikae vizuri. Wajua sina mtoto kwa hiyo mimi nataka nizae na Mondi.

Naskia Zari anataka kurudi, akirudi tutapambana, tutakuwa wake wenza, tutalea watoto wote.” Alieleza Lulu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments