6/25/2020

Rais Ampongeza Bilionea Mpya wa Madini


Rais John Magufuli amempongeza mchimbaji mdogo wa madini, Saniniu Kurian Lazer  ambaye leo ameiuzia serikali madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilogramu 15 na thamani ya Sh bilioni 7.74.

Ametoa pongezi hiyo alipompigia simu Waziri wa Madini, Dotto Biteko wakati serikali ikikabidhiwa madini ya Tazanie yenye thamani ya Sh bilioni 7.8 iliyoyanunua kwa mchimbaji Laizer.

“Hongera Laizer, najua unakwenda kutafuta mwanamke mwingine ukatafute mke wa Kisukuma,” amesema Magufuli wakati akizungumza na bilionea huyo.

Katika madini hayo, Jiwe moja lenye uzito wa kilo 9.2 lina thamani ya Sh bilioni 4.5 na lingine lina uzito wa kilo 5.8 lenye thamani ya Sh bilioni 3.3.

 Aidha Waziri Biteko amesema Laizer ameyatoa mawe hayo umbali wa mita 1,800 kutoka usawa wa ardhi ambapo Rais Magufuli aliagiza serikali inunue madini hayo.

Serikali tayari imemkabidhi Laizer mfano wa hundi ya Sh bilioni 7.744 na kwamba fedha hizo zitawekwa kwenye akaunti yake.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger