6/19/2020

Rasmi: Harmonize Ageukia UbungeSTAA wa Bongo Fleva, Rajab Abdul maarufu Harmonize, amesema ana mpango wa kugombea Ubunge katika Jimbo la Tandahimba Mkoani Mtwara, ikiwa ni miezi kadhaa baada ya Rais Magufuli kupendekeza afanye hivyo.

Amesema alijisikia furaha na faraja sana kuambiwa hivyo na Rais Magufuli kwa sababu sio kitu cha kawaida Kiongozi wa nchi kumpendekeza raia kugombea jimbo fulani na hiyo ilikuwa ishara na kuaminiwa.

Oktoba 2019 baada ya kutumbuiza katika mkutano wa hadhara Mkoani Lindi, Rais Magufuli alisema kuwa anatamani kumuona Harmonize akigombea Ubunge Tandahimba.

Endapo akagombea na kushinda, ataingia kwenye orodha ya wasanii ambao ni/ wamewahi kuwa wabunge nchini ambao ni pamoja na Joseph Haule (Profesa Jay), Joseph Mbilinyi (Sugu).HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger