6/23/2020

RPC na Mkuu wa TAKUKURU Waponea Tundu la Sindano fagio la Magufuli ArushaKamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana, na Mkuu wa TAKUKURU Arusha, Frida Wikes wameponea tundu la sindano kuondolewa madarakani na Rais John Magufuli ambapo amewapa onyo la mwisho.

Sababu kuu iliyowaweka matatani ambayo imebeinishwa na Rais Magufuli leo alipokuwa anawaapisha viongozi wapya Ikulu jijini Dar es salaam wakiwepo wa mkoa wa Arusha, ni kufanya kazi ambazo hajawatuma yeye.

Rais Magufuli amesema “IGP na Mkurugenzi wa TAKUKURU mko hapa, mkawaambie watendaji wenu walioko Arusha wafanye kazi nilizowatuma, nao leo nilikuwa niwatoe ambao ni RPC na Mkuu wa TAKUKURU wa Arusha”

Amesisitiza “Nimeamua kuwasamehe lakini sijawasamehe moja kwa moja wakifanya kosa lolote wataondoka. Wakafanye kazi nilizowatuma wasifanye kazi wanazojituma wao, haiwezekani watu umewatuma kufanya kazi za serikali wanafanya kazi wanazozijua wao”
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger