Tessy Aipa Kisogo Skendo Ya Kufumaniwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




MREMBO ambaye ni mzazi mwenza na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay Isahaka ‘Aslay’, Kaitesiya Abdul ‘Tessy’ amesema kuwa maisha yake yanaendelea kama kawaida tofauti na watu wanavyomuongelea kwenye mitandao ya kijamii.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Tessy alisema kuwa kuna mambo mengi yameongelewa kuhusu yeye kudaiwa kufumaniwa na mume wa mtu, lakini aliamua kukaa kimya kwa sababu ndilo jambo la busara siku zote na mwisho wa siku anaendelea na maisha yake.

 

“Wameniongelea sana vibaya lakini dawa kubwa niliyoitumia ni kunyamaza na kuwaangalia tu na mpaka sasa naendelea na maisha yangu ya kawaida, kwani walinisema mengi sana na yakapita na hata lile limepita kwa sababu tu mimi sio mtu wa kusikiliza maneno ya watu wanaotamani uanguke,” alisema Tessy bila kuweka wazi kuwa ni kweli alifumaniwa au la
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad