6/07/2020

Usiyoyajua Juu ya Maisha ya Mende ‘Anaweza Kuishi Bila Kichwa’


Mende ni mdudu anayeweza kuishi zaidi ya mwezi bila ya kula chakula chochote kutokana na kuwa ni mdudu mwenye damu ya baridi.

Mdudu huyu anaweza kuishi zaidi ya mwezi mmoja bila ya kula chakula chochote na ni mdudu anayeweza kuishi wiki moja bila ya kunywa maji.

Anakadiriwa kuwa ni mdudu ambaye amekuwepo katika uso wa nchi kwa muda mrefu kwa makadirio ya zaidi ya miaka milioni 350 iliyopita.

Wakati moyo wa mwanadamu ni mmoja wenye chemba nne mende ana moyo mmoja wenye chemba kumi na tatu na ni tofauti na wadudu wengine.

Mende haitaji kichwa ili aweze kuishi, ukimkata mende kichwa anaweza kuendelea kutikisa miguu yake hata  kwa wiki 1 au zaidi bila kichwa.

Hii ni kutokana na kuwa na vitundu vya kupumulia kwenye kila sehemu ya mwili wake, ambavyo vinamsaidia kuendelea kuishi.

Mende ana uwezo wa kukaa kwa zaidi ya dakika 40 bila ya kupumua na pia anaweza kuzama ndani ya maji na kuendelea kuwa hai kwa dakika 30. Mara nyingi huzuia pumzi yake ili kuzuia upotevu wa maji mwilini


Kuna takriban aina 4,600 za Mende lakini aina 30 ndizo huonekana sana karibu na binadamu na kati ya hizo 30 aina 4 tu ndiyo maarufu sana.

Miongoni mwa spishi zinazofahamika sana ni mende wa America, ambaye ana urefu wa milimita 30, mende wa ujerumani mwenye urefu wa milimita 15, na mende wa Asia anayekaribia urefu wa milimita 25. Mende wa kisasa ni wakubwa kidogo kuliko mende wa kale.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger