Uzee Wampa Mawazo WEMA Sepetu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



STAA asiyechuja miaka nenda rudi, Wema Sepetu amefunguka kuwa hakuna kitu anachokiwazia kwenye maisha yake kama maisha ya uzee na ndiyo maana ameona aanze kujiandaa mapema.

Akizungumza na Risasi Jumamosi hivi karibuni, Wema alisema huko nyuma alikuwa akidhani kuwa maisha hayasogei na umri hauendi, lakini ukweli ni kwamba, kila kitu kinaenda mbele na amegundua hata yeye atapita, watakuja mastaa wengine.


“Sitaki kuwaficha, uzee unaninyima usingizi sana, kuna wakati nawaza kabisa nikiwa mzee nitakuwaje mimi, najua wazi siku si nyingi watatokea Wema wengine, hivyo nimeona ni vizuri kuacha alama nzuri kwa mashabiki zangu na watu wengine maana kuna umri ukifika, vitu vyote unaviacha,” alisema Wema.

Stori:Imelda Mtema
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad