Vanessa Mdee Atangaza Kuacha Muziki “Tasnia Imejaa Mapepo”Baada ya kutangaza kupumzika kwa muda kufanya Muziki mwanadada Vanessa  Mdee amesema sasa anaacha rasmi tasni ya Muziki kutokana na matendo yaliyomo kwenye tasnia hiyo.

Akizungumza kwenye kipindi chake cha radio mtandaoni (podcast) Vanessa  amesema tasnia ya muziki imejaa mambo ya ajabu yasiyoaminika machoni pa watu.

“Kilichonifanya nichukue likizo kwenye muziki ilikuwa ni kuchagua maisha yangu na muziki unajua unapoingia kwenye tasnia watu wanakuambia upande mmoja tu wa mazuri na kusahau mabaya, kiukweli tasnia ya muziki imejaa mabaya mengi na ilibidi nichague kundelea kwenye ubaya au maisha yangu” amesema Vanessa  kwenye kipindi chake hicho chenye dakika 29.

“Najua mashabiki zangu watajiuliza kwamba sasa itakuaje je sitoimba tena, sitokuwa jukwaani kuwafurahisha ngoja niweke hili sawa napenda kuimba, na hiki ndicho kitu nililetwa duniani kukifanya nadhani kwa sasa nitabaki kuwa mwanga tu kwa wengine” ameongeza Mdee.

Ikumbukwe kuwa kwa sasa Vanessa yuko nchini Marekani akiishi na mwenzi wake Rotimi ambaye ni muigizaji pia muimbaji.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments