6/24/2020

Viongozi Wa Arusha Waliosamehewa na JPM Wahamishwa VituoViongozi wa Mkoa wa Arusha waliosamehewa na Rais Magufuli wakati alipotengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Jiji hilo wamehamishwa vituo vya kazi.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoani humo, Frida Wikes amehamishiwa Makao Makuu na Kamanda wa Polisi Mkoa, Jonathan Shanna amehamishiwa katika Chuo cha Polisi (CCP) Mkoani Kilimanjaro.

Aidha, inaelezwa kuwa mwingine aliyeathirika na uhamishaji huo ambao unaelezwa kuwa na lengo la kuongeza ufanisi katika utendaji kazi ni Mkuu wa Usalama Mkoa Arusha.

Hivi karibuni, Rais Magufuli alitangaza kuwasamehe Kamanda Shanna na Mkuu wa TAKUKURU Arusha kutokana na kufanya kazi tofauti na alizowatuma, ingawa aliweka wazi kuwa hajawasamehe moja kwa moja


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger