Virusi vipya vya mafua vyabainika kwa nguruwe nchini China

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Wanasayansi wamebaini uwepo wa aina mpya ya virusi vya nguruwe vinavyosababisha mafua  nchini China ambavyo vinahofiwa kuwa huenda vikasababisha janga la dunia.

Wataalamu hao wamesema virus hivyo vilivyobainika karibuni vinapatikana kwa nguruwe, na imeelezwa kuwa kuna uwezekano vinaweza kuongezeka kwa haraka na kuhamia kwa binadamu.

Licha ya kuwa hadi sasa havijawa tishio, lakini imeelezwa kuwa kuna dalili zote kuwa vinaweza kuathiri binadamu, hivyo kuhitaji ufuatiliaji wa karibu.

Kutokana na upya wake, virusi hivyo vitakuwa changamoto kwa sababu miili ya watu itakuwa na uwezo mdogo au kutokuwa na uwezo kabisa wa kukabiliana navyo.

Tishio hilo jipya limekuja wakati dunia ikiwa bado inaendelea kupambana na janga la virusi vya corona  
 
Aina mpya ya mafua iliyobainika nchini China ina ufanano kiasi na mafua ya nguruwe ya mwaka 2009, lakini kwa kiasi fulani yanatofautiana.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad