6/18/2020

Young Dee Afunguka "Nilipoanza Muziki Nilitaka Kuwa Kama MR Blue...Yeye Ndio Alinifungulia Milango"

Young Dee Ameandika haya:


Nilipokuwa najifunza kuimbaimba nikiwa mdogo sana, ndoto yangu ilikuwa kuwa kama @mrbluebyser1988! Nilikuwa natamani unyamwezi wake, style yake, mafanikio yake, alikuwa ndio kama kioo changu! Nilitamani siku moja walau nikutane nae nikiamini kwamba kukutana nae kungenifungulia mwanga wa sanaa yangu, kwani ningejifunza kuanza nikiwa mdogo kama alivyofanya yeye:

Mwaka 2003 nikiwa darasa la Tano, shule ya msingi Tabata Kimanga kipindi hicho nikiwa nachana chana tu darasani, washkaji zangu waliniambia kwamba Mr. Blue amehamia Tabata, na jioni hupenda kukaa sehemu flani karibia na shuleni kwetu, wakanisihi nifanye jitihada za kumtafuta Kwani atanisaidia kutoboa kimuziki.
Tulifanya jitihada mbali mbali, na siku moja tulifanikiwa kuonana na Blue, akiwa na kina Abby Skills. Nilichana mbele yake kwa aibu aibu, nikiwa na wasiwasi mkubwa kwasababu Blue alikua wamotoooo na bonge moja la bishoo, kuweza kupata ujasiri mbele yake ilikuwa changamoto kidogo.

Cha ajabu Blue aliona uwezo wangu pale pale, akanambia nifanye mazoezi zaidi kuweza kuboresha uwezo wangu. Kikubwa ambacho sitakaa nisahau kuhusu brother wangu huyu, ni namna alivyolichukulia swala lile kwa ukubwa, kwani aliniambia niende kwao Weekend iliyofatia, kuna CD ya beat nikafanyie mazoezi pale ajaribu kunirekebisha. Hamuwezi amini washkaji zangu, kitendo cha mimi mtoto wa kawaida kabisa kukubalika na Blue hadi kuingia nyumbani kwao Blue na kunisikilizisha beats, na kubond kama watu tuliokuwa tunajuana kitambo, ilinifundisha kitu kikubwa sana kuhusu thamani.

Long Story short, Blue aliweza kuniweka kwenye njia nzuri kimuziki. Safari yangu kimuziki ilianzia mikononi mwake. Alihangaika kutafuta maproducer wengi ili waweze kunirekodia nyimbo zangu bila mafanikio (ahadi zilikuwa nyingi), lakini hatimaye alinipeleka Dhahabu Record ambapo nilifanikiwa kurecord wimbo wangu wa kwanza kabisa katika maisha yangu, ambao ndio wimbo ulionitambulisha miongoni mwenu.

Brother Blue, kwa chochote nifanyacho leo, kilianzia kwenye hatua zile za Tabata, mchango wako kwenye sanaa yangu nitauthamini milele, bila wewe huenda ningepitia njia tofauti kufika hapa leo, na huenda isingekuwa nyepesi na yenye manufaa kama nilivyopitia kwako.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger