7/16/2020

Account za Watu Maarufu Wakiwemo Bill Gates na Baraka Obama Zadukuliwa TwitterAkaunti za Twitter za watu maarufu duniani wakiwemo Elon Musk, Barack Obama, Kanye West na Bill Gates zimedukuliwa katika kashfa inayohusisha fedha za kidijitali mtandaoni ya Bitcoin
-
Akaunti za Gates na Musk zilituma ujumbe uliowataka watu kutuma Dola 1,000 na kusema watarudishiwa Dola 2,000. Msemaji wa Bill Gates amezungumiza tukio hilo akisema Bilionea huyo hakutuma ujumbe huo
-
Mwanzilishi wa #Twitter, Jack Dorsey amesema imekuwa siku ngumu kwao na wanasikitishwa na kilichotokea. Ameongeza kuwa, wanachunguza na taarifa zaidi zitatolewa wakifahamu kilichotokea
-
Hii sio mara ya kwanza kwa akaunti za Twitter kudukuliwa. Mwaka 2018 akaunti za Target na G-Suite ya Google ambazo zilikuwa zimethibitishwa na mtandao huo zilidukuliwa


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger