7/16/2020

Mfahamu MTU Mweusi wa Kwanza Kufanyiwa Upandikizaji wa Uso....Julai mwaka huu,Robert Chelsea alifanikiwa kufanyiwa pandikizi la uso mzima,akiwa ni Mmarekani mweusi wa kwanza duniani na mtu wa 40 kwa ujumla tangu mapandikizi ya namna hii yaanze kufanyika mwaka 2005.

Upandikizwaji wa sasa aliofanyiwa ndio unaonekana kuwa na mafanikio makubwa zaidi,ulifanyika kwa saa 16 chini ya uangalizi wa timu ya madaktari 45.Aliipata ajali hii mwaka 2013 baada ya gari yake kuparamiwa na gari lingine ambalo dreva wake alikuwa kalewa pombe hivyo kumsababishia apoteze uso wake pamoja na sehemu zingine nyingi za mwili wake.

Baada ya kufanyiwa upasuaji kwa zaidi ya mara 30 bila mafanikio,Julai ya mwaka huu inaweza kuwa ya matumaini makubwa kwa bwana Robert Chelsea ambaye hadi sasa anaendelea vizuri.Alifanyiwa huduma hii Boston's Brigham and Women's Hospital

=> Usisahau Kulike, Kucomment na Kushare na Marafiki.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger