7/17/2020

Aston Villa yapoteza matumaini kubaki ligi kuu ya UingerezaKlabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu Uingereza ambapo nyota Mtanzania, Mbwana Samatta anakipiga imepoteza matumaini ya kubaki ndani ya Ligi hiyo baada ya sare ya kufungana bao 1-1 na Everton hapo Jana. 

Mchezo huo ulikuwa na maana kubwa kwa #Villa endapo wangeshinda na kusepa na pointi tatu, ambapo wangejiongezea nafasi ya kubaki ndani ya ligi hiyo. 

Wachezaji na benchi la ufundi baada ya mchezo huo hawakuwa na furaha kwa kuwa waliyeyusha matumaini ya kubaki msimu ujao wa 2020/21. 

Sare hiyo inaifanya #Villa ibaki nafasi ya 19 ikiwa na pointi 31 huku #Everton ikiwa nafasi ya 11 na pointi 46 zote zimecheza mechi 36. 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger