7/26/2020

Bethidei ya Kajala Yamuibulia Jambo P- Funk


MJINI kuna mambooo! Juzi (Jumatano), Sinza jijini Dar es Salaam, kulikuwa na sherehe ya ‘bethdei’ ya msanii wa filamu nchini Kajala Masanja, lakini katikati ya shughuli likazuka jambo, tega sahani upakuliwe ubuyu.

Jambo lenyewe linamhusu prodyuza mahili Bongo, Paul Matthysse ‘P- Funk’ ambaye ni mzazi mwenzake na Kajala, kujikuta akipata ‘wenge’ baada ya kile kinachotajwa kuwa ni mkewe wa sasa (jina kapuni) kumaindi uwepo wake kwenye shughuli hiyo.

Waandishi wetu ambao walikuwepo kwenye shughuli hiyo iliyoandaliwa na Meneja wa Kajala, Leah Mwendamseke ‘Lamata’ kama sapraiz kwa msanii huyo, walishuhudia sapraiz nyingine baada ya mzee baba P- Funk kuibuka shughulini.

Baada ya kutimba kibabe kwenye sherehe hiyo, prodyuza huyo alikwenda moja kwa moja kwa EX wake na kumkumbatia ambapo ‘mama’ naye alionesha mahaba kwa kukata keki na kumlisha mzazi mwenzake.

Kitendo hicho cha P-Funk, kiliibua shangwe kwa wageni waalikwa waliokuwa wameshiriki shughuli hiyo iliyofanyika ndani ya ofisi ya Kajala iliyopo Sinza Afrikasana.

Waandishi wetu walipomuuliza prodyuza huyo ana ujumbe gani kwa mzazi mwenzake kwa siku yake ya kuzaliwa, alisema:“Namtakia kila la kheri katika siku yake muhimu ya kuzaliwa, lakini pia nafurahi kuona ana ofisi yake, nadhani amekuwa mtu mzima sasa,” alisema P- Funk na kushangiliwa na watu.

P- FUNK APOKEA SIMU

Hata hivyo, wakati shughuli ikiendelea, ghafla prodyuza huyo alipigiwa simu na mtu anayedaiwa kuwa ni mke wake akimhitaji arudi nyumbani.Chanzo cha karibu na P- Funk kiliwanong’oneza waandishi wetu kuwa, kuna wambeya kutoka shughulini hapo walikuwa wamerusha klipu ya video mtandaoni ikimuonesha Kajala na mzazi mwenzake huyo wakiwa wamekumbatiana jambo ambalo linadaiwa kumkera mke wa P- Funk.

“Ameona hizo video na kujisikia vibaya, amempigia simu mumewe huku akilia na kumwambia arudi nyumbani haraka.“Unajua leo pia ni kumbukumbu ya kuzaliwa ya mtoto wa mwisho wa P- Funk, sasa mke kamuona mumewe kwenye sherehe nyingine kapagawa,” chanzo kilisema

P-FUNK AAGA

Aidha, baada ya P- Funk kumaliza kuongea na simu, waandishi wetu walimshuhudia prodyuza huyo akiwaaga baadhi ya waalikwa na kuwaambia kuwa anakwenda kwenye sherehe ya mtoto wake wa mwisho na kuahidi kurejea tena baadaye.


KUMBE KAJALA ANA MIAKA 37


Mbali na yote, jambo lingine lililozua gumzo katika shughuli hiyo ni umri wa Kajala kuonekana mkubwa tofauti na jinsi anavyoonekana.“Jamani, kumbe Kajala ana miaka 37? Yaani haendani kabisa; ukimuangalia utadhani ana miaka 30,” mwalikwa mmoja alisema.


 


Hata hivyo, waandishi wetu walipomuuliza Kajala usahihi wa miaka yake, alisema bila kupepesa macho:“Unajua mimi nilimzaa Paula (mtoto wa P-Funk) nikiwa na miaka 19, hivyo mwaka huu binti yangu katimiza miaka 18, kwa hiyo leo nimetimiza miaka 37.Baadhi ya wasanii kama Aboot Rack ‘Quick Rocka, Asha Mzuzuri ‘Asha Boko’ na wengineo, walikuwepo kwenye sherehe hiyo ya kuzaliwa msanii huyo ambaye amekuwa na bifu na msanii mwenzake Wema Sepetu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger