Corona Afrika Kusini yawa tishio, watu 572 wapoteza maisha ndani ya saa 24


Kuna wasiwasi kuwa huenda idadi ya waliopoteza maisha kutokana na virusi vya corona ni kubwa zaidi kuliko takwimu zinavyoonesha.

Watu 572 wamepoteza maisha kutokana na virusi vya corona kwa kipindi cha saa 24 zilizopita.

Lakini watafiti kutoka baraza la utafiti wa tiba nchini Afrika Kusini wamesema kuwa idadi ya waliopoteza maisha ni kubwa zaidi kuliko kawaida- wakisema kuwa maelfu ya vifo vitokanavyo na Covid-19 huenda havikuripotiwa.

Mpaka sasa, takwimu rasmi zinaonesha, karibu watu 6,000 walipoteza maisha kutokana na Covid-19.

Lakini tafiti za majuma kumi yaliyopita zinaonesha kuwa kumekuwa na vifo 17,000 zaidi kuliko kawaida.

Watafiti wanasema kuna vifo 11,000 ambavyo havijaelezwa.

Wanakisia kuwa vingi kati ya hivyo inawezekana kuwa vinahusiana na Covid-19 kama wale waliopoteza maisha wakiwa nyumbani na vifo vingine ambavyo havijaripotiwa.

Lakini kumekuwa na maoni kuwa raia wa Afrika Kusini wanaepuka kwenda hospitali- kwasababu hakuna nafasi, au wasiwasi wa kupata maambukizi

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments