Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Corona Kenya: Vifo, Wagonjwa Waongezeka

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


IDADI ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa wa Covid-19 nchini Kenya inakaribia 300 kulingana na takwimu zilizotolewa na serikali Jumanne.

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe, alitangaza kwamba watu wengine 14 wamefariki kutokana na virusi hivyo katika kipindi cha saa 24 na kufanya idadi ya waliofariki kufikia sasa kuwa 299.
 
Aidha idadi ya wagonjwa waliothibitishwa kuwa na maradhi hayo imefikia 18,581 baada ya waziri wa afya kutangaza wagonjwa wengine 606.

Kati ya wagonjwa hao wapya 583 ni raia wa Kenya huku 23 wakiwa raia wa kigeni, wanaume wakiwa 409 nao wanawake wakiwa 197. Mgonjwa mwenye umri mdogo zaidi ni mtoto wa miezi minne huku mtu mwenye umri mkubwa zaidi akiwa mzee wa miaka 85.

Hata hivyo, habari njema ni kwamba wagonjwa 75 wa corona wamepona maradhi hayo, na kufanya jumla ya waliopona nchini Kenya kufikia 7,908. Wagonjwa hao wanatoka katika maeneo tofauti.


Idadi ya wagonjwa kulingana na kaunti

Nairobi imeandikisha wagonjwa 448, Kajiado 25, Machakos 16, Uasin Gishu 11, Nakuru 11, Kericho 9, Busia 7, Mombasa 7, Garissa 6, Bomet 3, Nyeri 2, Narok 2, Nandi 2, Embu, Lamu, Murang’a zikiwa na wagonjwa mmoja-mmoja.Mjini Nairobi eneo la Embakasi limetajwa kuwa na wagonjwa wengi na waziri huyo amewataka wakazi wake kuchukua tahadhari. Kagwe amewataka wale wanaofanya kazi kutoka nyumbani kujaribu kufanya kazi katika nyumba zao.”Nimekuwa risasi, umekuwa risasi . Tunaweza kumuua mtu, Tumekuwa hatari,” alisema. Amewataka wazazi kuwasisitizia watoto wao kuosha mikono, kupaka sanitizer na kuchukua kila tahadhari.

Post a Comment

0 Comments