Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Covid19: Masista 12 Wafariki Kwenye Parokia Moja, Wengi Waambukizwa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREWaliofariki walikuwa kati ya umri wa 79 na 99 wengi wakiwa walimu. Picha: Hisani.

Kulizuka mlipuko wa covid katika parokia ya Felican Michigan, USA

Kwa muda wa mwezi mmoja, watawa 12 walifariki kutokana na virusi hivyo

Waliofariki walikuwa kati ya umri wa 79 na 99 wengi wakiwa walimu

Zaidi ya watawa 12 wamefariki baada ya kuambukizwa virusi hatari vya corona katika parokia moja, Michigan Amerika.

Masista hao waliokuwa wakiishi pamoja katika parokia ya Felican eneo la Livonia walikuwa na umri wa kati ya 79 na 99.

Watawa hao wameripotiwa kufariki kati ya Aprili, 10 na Mei 10 kutokana na virusi hivyo.

Hadi Mei 10, takriban masista 18 walikuwa wameambukizwa kabla wengine 2 kufariki Juni 27 kama ilivyoripotiwa na jaridala Siters Global Report.

Wengi wa watawa hao waliofariki walikuwa wakifanya kazi kama walimu na wauguzi katika parokia hiyo ya Livonia iliyokuwa nyumbani kwa watawa 65 kabla kuzuka virusi hivyo.

12 nuns from one convent succumb to COVID-19 within a month, dozen others ill

‘’Ilianza na wauguzi wawili. Hatukujua walikuwa kina nani na hatukutaka kujua. Kisha iliwaambukiza masista katika orofa la pili na kuenea kama moto,’’ Mary Andrew. Kiongozi wa masista hao alisema.

Andrew ambaye pia aliambukizwa virusi hivyo na kupona muda baadaye alieleza kuwa hawakuambiwa majina ya masita walioangamia. Walikuwa wakiambiwa kuwa moja zaidi amefariki bila kutambulishwa jina.

‘’ Hata hawakuwa wanatumbia idadi, walikuwa wakisema mwengine tena amefariki, sista mwengine amefariki, Mary Andrew aliongezea.

Alisema kuwa maambukizi ya virusi hivyo vimewatia hofu kubwa na kuwa hawawezi kukutana  tena kama kikundi hata kufanya maombi.

Post a Comment

0 Comments