Dawa ya HIV imepatikana? Wanasayansi waonya kuhusu kusherehekea mapema baada ya jamaa mmoja kudaiwa kupona HIV Brazil

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 36 nchini Brazil huenda akawa mtu wa kwanza kupona  HIV bada ya kutubiwa kwa mseto wa dawa za  kukabiliana na virusi hivyo ,watafiti wamesema .

 Ni watu wawili pekee ambao wamethibitishwa kupona ugonjwa huo baada ya matibabu yanayofanywa kwa njia ya kitaalam na hatari sana  yalihusisha  kuondolewa  kwa ‘Bone marrow’  kutibu kansa zinazozuka baada ya ugonjwa huo kukithiri mwilini .

Mgonjwa huyo Brazil hajaonyesha daalili za  maambukizi ya HIV  baada ya kufanyiwa vipimo vya damu  kulingana na watafiti katika chuo kiku cha  Sao Paulo kinachotambulika kwa tafiti za hali ya juu .

Wamesema kisa hicho ni cha mwanzo na majaribio ,huenda ndicho cha kwanza kwa matibabu ya kudumu ya mtu aliyeambukizwa HIV .

 Lakini katika mataifa mengine watafiti wametaka pawepo tahadhari katika kuanza kutangaza ushindi wa mapema dhidi ya HIV . Dr Steve Deeks  ambaye ni mtafiti wa HIV kutoka  chuo kikuu cha California amesema  ukosefu wa  antibodies katika mgonjwa huyo ni jambo la kushangaza katika kisa hicho  na utafiti zaidi unafaa kufanywa kubaini hali hiyo ndiposa pawepo uhakiki wa kupatikana kwa tiba ya kudumu ya HIV .

Deek amesema ni mapema sana kujua iwapo mgonjwa huyo wa Brazil ana ukimwi hadi matokeo hayo yathibitishwe na  maabara huru
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad