7/17/2020

Fahamu Kisa cha Aliyeahirisha Kuwania Ubunge


Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Kulwa Mang'ana, amepata ajali katika eneo la Boman'gombe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, wakati akiwa njiani kuelekea Wilaya ya Siha kwa lengo la kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge kupitia CCM, ambapo baada ya ajali aliahirisha nia yake hiyo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ilitokea jana Julai 16, 2020, majira ya saa 10:00 jioni njia panda ya kuelekea Siha, ambapo dereva wa Pikipiki aliigonga gari yake kwenye eneo la mlango wa dereva na kusababisha kuvunjika kwa kioo ambacho vipande vyake vilimuingia sehemu za mwili ikiwemo kichwani.

Mara baada ya ajali hiyo kutokea, mtia nia huyo alieleza kusitisha zoezi la kwenda kuchukua fomu huku akiwatakia kila lenye heri wote waliojitokeza kuchukua fomu katika Jimbo hilo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mstaafu Aggrey Mwanry na Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel.

Na kwamba ameamua kuachana na dhamira hiyo kwa kile alichodai kuwa viongozi hao, wamewatumikia vyema wananchi na kuaminiwa na  Rais Magufuli, hivyo ameona wanatosha na yeye atangoja hadi mwaka 2025.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger