7/30/2020

Fatma Karume Ahoji Zanzibar Kupiga Kura Wakati Rais Ameanza KutangazwaAliyewahi kuwa rais wa chama cha wanansheria Tanganyika (TLS) Fatma Karume amehoji ni kwa nini Uchaguzi mkuu visiwani zanziba ufanyike ilhali shirika la utangazaji nchini (TBC) limentaja Dkt Hussen Mwinyi kuwa rais mteule wa Zanzibar.

Karume amehoji hayo kupitia ujumbe alituma lwenye ukurasa wa twitter na kuongeza kuwa kitendo cha kumtanga Mwinyi kama rais mteule ni kuvunja katiba.

“Kama Hussein ni Rais Mteule wa Zanzibar ya nini kupiga kura Oct 2020. Si wamtangaze tu? Wanasubiri nini? Kipindi cha Shein kimalizike? Wanaheshimu kipindi kilicjowekwa na katiba yetu? Kama Katiba yetu haiheshimiwi na tunabandikizwa Rais mteule basi wamuapishe tu” ameandika Fatma Karume.

Dkt Hussein Mwinyi ameteuliwa na mkutabo mkuu wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) manamo Julai 10,2020 jijini Dodoma kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Oktoba.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

1 comment:

  1. Fatma, Hujaelewa na haukusikia vyema.

    ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger