7/31/2020

Fatma Karume Amelicharua Jeshi la Polisi na Kuwaambia Tusitishane Kabisa


Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume amesema alilalamika kuhusu jengo lake kupigwa bomu na hakuna majibu yoyote aliyopewa hadi sasa.

Jana jeshi la polisi limemtaka mtu yoyote ambaye anahofu na usalama wake kutoa taarifa hizo polii ili ziweze kufanyiwa kazi badala ya kulalamika mitandaoni na kwenye vyombo vya habari vya ndani na nje.

“Mimi nimelalamika kuhusu jengo langu kupigwa bomu. Nimeenda mpaka kwa DCI pale HQ Wizara ya ndani @ tanpol mpaka hii leo hamjanipa majibu yoyote,” aliandika Fatma katika ukurasa wake wa twitter

“Bado mnataka nikae kimya ili iweje? nitalalamika tu kwamba hamjanipatia majibu yeyote wala hamjakamata mtu. tusitishane kabisa,”
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger