7/18/2020

Hakika Bernard Morris ni Mkubwa Kuliko YANGA....Aendelea Kuwaumiza Kichwa Viongozi Wadai Aondoke Aone

 
Uongozi wa klabu ya soka ya Yanga umesisitiza kwamba kwa sasa hauhitaji kuzungumzia masuala ya mkataba baina yake na Benard Morrison kwa kuwa kila kitu kipo wazi na iwapo anasema hajasaini basi aende katika klabu inayomhitaji.


Tamko hilo limetolewa na mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa timu hiyo Hassan Bumbuli ambaye amesema hawana muda wa kupiga porojo juu ya suala la mchezaji mmoja ambaye ameripotiwa akisema anadai mshahara wa miezi miwili.

''Yeye anasema anatudai ataoe risti ambazo zinamuonyesha hatujamlipa namshangaa sana ache kuwasumbua watu yeye kama anataka kuondoka aendee tu kabla ya dirisha  la usajili alijafungwa'', amesema Bumbuli.

Katika hatua nyingine Bumbuli amesema wataendelea kumchukulia hatua kwa kila kosa analolifanya kupitia kanuni za kinidhamu,na wao hawana mpango wa kumbembeleza kurejea kikosini kwa kuwa yeye hawezi kuwa mkubwa zaidi ya Yanga.

Morrison amekua akihusishwa kwa utovu wa nidhamu, ikiwemo kuukana mkataba wa miaka miwili unaotajwa ameusaini,lakini pia majuzi aliondoka uwanjani baada ya kufanyiwa mabadiliko katika dabi dhidi ya Simba na mpaka sasa haijulikani anapoishi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger