Hali ya Kuogopa Kisichokuwepo Inanitesa. Ni Mimi tu Ama Tupo Wengi


Ebwana niaje..

Hali ya kuogopa kisichokuwepo inanisumbua sana kiasi kwamba inakera na kuathiri hata mienendo yangu...

Ipo kama hivi.. Mfano nipo kwenye nyumba ambayo nje kuna mti mkubwa nakosa amani nahisi mti utaangukia nyumba..

Nikienda uwani(chooni) lazima nimulike tundu ama kuflash kabisa hata kama safi.. Haipiti sekunde nne tano bila kuangalia yaan nahisi kama nyoka anataka kunimega kalio..

Sipendi kukaa mbele ya dirisha nahisi kuna mtu atanichokoa na chuma au mti..

Kukaa chini ya mti nahisi nyoka atadondoka sasaivi...

Nikipewa ahadi hata kama ni saa moja tu mbele linakuwa refu kwelikweli nahisi kama jamaa ataghairi..

Mke wa mtu sasa eti naogopa kunasa..

Eti kulala na kahaba nitapata ngoma.. Hii inanifanya nisdhubutu hata nawaona watu wanaonunua hawa viumbe wana roho ngumu sana..

Mtu wa karibu akiumwa moyo hautulii eti atakufa sasaivi huyu...

Siku zote naomba nisiishi nyumba iliyo pembeni ya barabara naona kabisa mda wowote lori litaivaa hii nyumba

Kuwa mbali ni mpenzi mda wote nawaza eti analiwa huko...

.. Fear for nothing ni mimi tu ama??? Yaani nakosaga amani nikiwa katika mazingira haya naogopa kitu hata hakipo..

Wajuzi wa mambo tufahamishane ni nini hiki...

Je ushawahi hofia kitu ambacho hakipo?

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

1 Comments

  1. Mko wengi. kwani na wewe Chaadema?

    M/kiti kasema 14Days. wewe umeendelea
    kujichimbia? posho mwanangu POSHO

    ReplyDelete