7/20/2020

Hatimaye Zitto Kabwe Atangaza Jimbo Atakalogombea UbungeKiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini anayemaliza muda wake Zitto Kabwe, ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo hilo kwa mara nyingine tena.


Kupitia Ukurasa wake wa kijamii wa ‘twitter’ Zitto ameandika kuwa huu ndio wakati muhimu kwa historia ya demokrasia na yuko tayari kugombea ubunge Kigoma mjini.

“Huu ni wakati muhimu zaidi katika historia ya demokrasia ya Vyama vingi nchini. Ni wakati wa kuhami demokrasia yetu. Ni wakati wa kuhakikisha tunaunda Serikali ili kurejesha furaha kwa Watanzania. Nimeamua kuwa Nitagombea Ubunge Kigoma Mjini”, ameandika Zitto.

Watia nia Ubunge Kigoma mjini mpaka sasa kupitia ACT-Wazalendo ni Zitto Kabwe, Abdul Nondo, Hussein Kaliango na Idd Adam
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger