Hii ni Shule ya Msingi Lupaso Aliyosomea Marehemu Rais Benjamin Mkapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hii ni Shule ya Msingi Lupaso, sehemu ambayo safari ya kutafuta maarifa ya Marehemu Rais Benjamin Mkapa ilianzia mwaka 1945.

Shule hii iliweka msingi imara na kumuwezesha kupita katika taasisi nyingine za elimu na kumuwezesha kukabidhiwa fungua za Ikulu ya Tanzania mwaka 1995, nafasi aliyoitumikia hadi mwaka 2005.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Charles Maduka amesema serikali imewapa shilingi milioni 400 kwa ajili kujenga shule, na walipanga kumualika Rais Mkapa kuja kuizindua.

Ameongeza kuwa kiongozi huyo alikuwa na mchango mkubwa katika elimu na kwa kutambua hilo eneo la darasa alimosoma kiongozi huyo patajengwa maktaba.

Kwa upande wake Mwalimu Tusuwege Kayinga amesema atamkumbuka Rais Mkapa kwa namna alivyowasaidia wafanyakazi kupata mikopo yenye riba nafuu ambayo amenufaika nayo. #BurianiMkapa
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad