7/16/2020

Huyu ndio Mrithi wa Paul Makonda Dar es salaam, anaitwa Aboubakar kunenge


Hizi ni ripoti kutoka Chamwino Dodoma Tanzania kwenye makazi mapya ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ambapo baada ya Paul Makonda kutangaza nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni na kuchukua fomu leo, Rais JPM amefanya uteuzi wa Mkuu mpya wa Mkoa.

Taarifa ikufikie kwamba Mkuu mpya wa Mkoa aliyeteuliwa leo ni Aboubakar Mussa Kunenge ambaye kabla ya kuteuliwa kwenye Ukuu wa Mkoa alikua ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam ambapo sasa Paul Mshimo Makanza ndio ameteuliwa kuchukua nafasi hiyo ya Katibu Tawala wa Mkoa.


Paul Makonda.

Kabla ya Paul Mshimo kuteuliwa kwenye ukatibu Mkuu alikua Afisa Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania ambapo mabadiliko haya yametokana na Paul Makonda kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Kigamboni Dar es salaam leo asubuhi
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger