7/29/2020

Ibada ya Hijja inaanza Leo kwa idadi ndogo ya Waumini wa Kiislamu


Makka, Ibada ya kila mwaka ya Hijja inaanza leo katika mji mtukufu wa Makka nchini Saudi Arabia chini ya kiwingu cha janga la virusi vya corona lililosababisha kupunguzwa kwa idadi ya watu watakaoshiriki ibada hiyo.

Waislamu wasiopindukia 10,000 ambao tayari wanaishi nchini Saudi Arabia ndiyo watashiriki Hijja inayofanyika kwa siku tano, idadi ambayo ni sehemu ndogo ya mahujaji milioni 2.5 waliohudhuria mwaka uliopita.

Vyombo vya Habari vya Taifa vimeonesha wafanyakazi wa afya wakipuliza dawa ya kupambana na virusi kwenye masanduku ya mahujaji huku wengine wakipatiwa mikanda maalum ya kufuatilia mahali waliko.Kwa lengo pia la kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona, mamlaka inayosimamia ibada ya Hijja pia imepiga marufuku kwa mahujaji kuligusa ´´Ka´bah´´ jengo dogo la mraba lililo katikati ya msikiti mkuu wa mjini Makka.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger