Inatisha..Wabunge 15 wa Zambia Wakutwa na Virusi vya Corona

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa Afya wa Zambia Chitalu Chilufya amesema baada ya zoezi la lazima la upimaji wa virusi vya corona katika bunge la nchi hiyo, wabunge 15 wamekutwa na maambukizi.


Amri ya upimaji huo ilitolewa baada ya wabunge wawili kufariki dunia juma lililopita. Mmoja miongoni mwa hao aliugua ugonjwa wa COVID-19, hadi kipindi hicho binge la Zambia lilikuwa na Wabunge 158. Katika hatua nyingine Msemaji wa Serikali ya Kenya Cyrus Oguna pia amethibitishwa kuwa na virusi vya corona. Katika ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa aliona dalili na kwa sasa anapatiwa matibabu katika eneo alilojitenga.


Nchini Afrika Kusini mawaziri wawili walifikishwa hospitali baada ya kupata maambukizi. Hadi wakati huu Zambia ina visa 3,584 vya

maambukizi, wakati Kenya 15,601. Shirika la Afya Dunia WHO hivi karibuni lilionya kutokana na kuchelea kuanza kwa mripuko huo barani Afrika visa vyake katika kipindi hiki vinaongezeka kwa kasi..

Rekodi kama hizi za sasa zilitokea mapema Juni ambapo lilirekodi vifo vya zaidi ya watu 1,000 kwa siku nne mfululizo, kulikotokana na kuzuka kwa kiwango kikubwa cha maambukizi cha Aprili. Kwa ujumla Marekani ina vifo 145,352 huku maambukizi yakipindukia watu milioni 4.

Mamlaka nchini Ujerumani zinampango wa kuweka vipimo vya virusi vya corona katika viwanja vyake vya ndege kwa ajili ya wasafiri ambao wanatoka katika mataifa yenye kitisho zaidi cha maambukizi hayo.

Uamuzi huo umefikiwa na maziri wa afya wa majimbo 16 ya Ujerumani unatokana na uwepo wa wasiwasi kwamba watu wanaorejea kutoka katika matembezi ya likizo ya  msimu huu wa kiangazi watarejesha virusi hivyo kutoka katika maeno watokako. Lakini pia kuna wasiwasi kwamba sio kila mtu, anaetoka katika maeneo yalioainishwa kuwa ya hatari anaweza kujitenga pasipo kufanyiwa vipimo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad