7/18/2020

Insta Pamechafuka Mwanamuziki Rayvanny na Bosi Wake Diamond Platnumz Watamba Kushika Number Moja Apple Music

Mnyama mkali kutoka WCB, Chui Rayvanny amezidi kufanya vizuri kimataifa mara baada ngoma yake ya "Amaboko" aliyomshirikisha Diamond Platnumz kushika namba moja kwenye mtandao mkubwa wa kuuza nyimbo duniani uitwao, Apple Music.

Ngoma mpya ya ayvanny ‘Amaboko’ imekua ndio nyimbo inayofanya vizuri zaidi kati ya nyimbo za Afrika zilizoachiwa hivi karibuni.

Sanjali na hilo, pia picha ya Rayvanny imewekwa kwenye Cover ya Playlist kubwa ya Muziki Barani Afrika (Africa Now).

Apple wamekua na utaratibu wa kuweka cover za Mastaa ambao Ngoma zao zinaongoza kwa Mauzo katika mtandao huo, kwenye Playlist zao mbalimbali.

Hivyo basi, Rayvanny anakuwa msanii wa kwanza Tanzania na Afrika Mashariki kwa picha yake kutumika Kama Cover katika Playlist hiyo kubwa zaidi barani Afrika kwa sasa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

1 comment:

  1. waongo, Nandi ndo msanii wa kwanza kuwa kwenye apple muzik. yaani hata aibu hawani..

    ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger