Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Jack Wolper Ajiweka kwa ‘Kitoto’

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


MLEZI wa wana? Ndivyo unavyoweza kujiuliza baada ya staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Masawe kujiweka kwa mara nyingine kwa mwanaume aliyemzidi umri (kitoto).

Wolper amevunja ukimya uliokuwa umetawala baada ya kuvishwa pete ya sintofahamu ya uchumba na Rashid Juma ‘Chid Designer’ kisha uchumba kuyeyuka.

Wolper ameibuka na na mpenzi mwingine anayejulikana kwa jina maarufu la Rich Mitindo.

Hivi karibuni, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilimnyatia Wolper na kumnasa laivu akiwa kwenye mahaba mazito kule mkoani Iringa.

Katika mahojiano na Wolper baada ya kunaswa kwenye malavidavi walipokuwa mkoani Iringa kumsindikiza Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kuchukua fomu ya ubunge, Wolper aliweka wazi kuwa kwa kipindi hiki amenasa kwa mtanashati huyo na hakuna wa kumwambia chochote.

Wolper alisema kuwa, watu wanaweza kumshangaa kuanzisha penzi hilo jipya kwa kipindi kifupi tangu afanyiwe mchezo mchafu na Chid Desgner, lakini ukweli ni kwamba Rich Mitindo ni mtu wake wa muda mrefu yapata miaka minne sasa.

“Najua watasema sana, lakini ukweli wa mimi na huyu Rich hawaujui kwamba ni mtu wangu wa muda mrefu sana na sasa nimeamua ukweli kabisa kutulia kwake nifanye naye maisha,” alisema Wolper na kusisitiza kwamba, pamoja na kufanyiwa lile tukio la kuvishwa pete na kuachwa ndani ya wiki moja, amelisahau kabisa.

Wolper anasema, hakuwahi kufikiria kuwa na mtoto kama wale wengine wote waliopita, lakini kwa Rich amefanya hivyo kwa kuwa anataka kutulia sasa.

“Kuna wakati nakuwa na mwanaume, lakini sifikirii hata kidogo kuhusiana na kuzaa, lakini kwa kipindi hiki nimefikiria hilo na Mungu atupe tu uzima, watu watashangaa sana,” anasema Wolper.

Anasema kuwa umri wake kwa sasa umesogea, hivyo anaona huu ndiyo wakati wa kuzaa na mwanaume wa kumuita baba mtoto wake ni huyu aliye naye kwa sasa.

“Kwa kweli huu ndiyo wakati wangu wa kuzaa na huyu ndiye baba sahihi kwa mtoto wangu kwa jinsi tu nilivyomuona na ninavyomjua. Hapa ndipo nimefika, nina shauku ya kupata mtoto kuliko kitu kingine,” alimalizia Wolper.

Ukimuacha yule ‘Mkongo wa Wolper’ na staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ waliompita umri wake wa sasa wa miaka 33, Wolper aliwahi kudaiwa kupita na wanaume wengine kama Jux, Diamond, Harmonize, Brown, Young Killer kisha Chid Desgner na sasa Rich Mitindo.

Post a Comment

0 Comments