7/24/2020

Je, Mzee Yusuph Atawapika Vijana Wapya au Atarudi na Vijana Wake Wale Wale?Miongoni mwa vitu vinavyosubiriwa kwa hamu kwa wapenzi wa burudani ya muziki ni ujio wa mfalme Mzee Yusuph.

Tangu mfalme akae mbali na muziki wa taarabu muziki huo ulikuwa unakaribia ukingoni kupotea /kufa kabisa.

Watu kama akina Omari Tego, Muhammed mtoto pori ,Prince Amigo ,nk japo walikuwa wakitoa nyimbo mbalimbali ,nyimbo zao hazikuwa zikisikika sana kwa sababu watu walikuwa wameshaachana na muziki huo .

Sasa mfalme anarudi kundini sasa, tunatarajia mambo mazuri mazuri katuandalia .

Lakini swali linakuja ,je mfalme atarudi na watu wake wale wale ah atapika vijana wapya??

Kipindi kile jahazi kilikuwa na wasanii moto moto sana ,tukianza na mtoto wa mfalme ,Prince Amigo, Mtoto pori, Miriam Amour, Mwasiti Mbwana (Kitoronto), Rahma Machupa (Messi) ,Fatma Nyoro, Khadija Yusuph, Mwanahawa Ally, malkia Leyla Rashid na Mfalme mwenyewe mzee Yusuph .

Hakika kipindi hicho ,ukisikia Jahazi, ujue Jahazi kweli .

Sasa tangu mfalme apumzike kidogo vijana wake wote walienda bendi mbali mbali ,mfano Father Mauji, Mwasiti ,Rahma Machupa na Mtoto pori waliunda bendi yao ya Naksh Naksh modern taarab.

Fatma na Khadija Yusuph wakaenda Yah TMK ambako waliungana na Maua Tego.

Abubakar Sudi (Prince Amigo ) yeye akaunda bendi ya First Class modern taarab.

Sasa kwa mwendo huu inakuwa vigumu kuwarudisha wasanii wote na kurejesha Jahazi ambapo kwa sasa imebadilishwa jina na kuita Safina Modern taarabu.

Ngoja tusubiri muongozo tuone itakuwaje maana mfalme ni kazi ndogo sana kwake kuwapika vijana wapya na wakawa wakali kuliko hata hao wengine.

Kama aliweza kuwapika hao kipindi hicho anahama Zanzibar Stars na kuanzisha bendi ya Jahazi basi bila shaka hatoshindwa kutuletea wasanii wengine wazuri zaidi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger