Je Wajua Kwanini Wanawake Hula Vyakula vya Ajabu Ajabu Wakiwa Wajawazito?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tabia hii inayojulikana kwa Kiingereza kama “Pica” inatokana na mtu kutamani kula vitu vyenye virutubisho kidogo sana au visivyo na virutubisho vya aina yoyote kwa mwili.

Tamaa hizi huwa zinawapata watoto au mama mjamzito kutafuna vitu ambavyo kimsingi si chakula – kama udongo au chaki. Jina hili la pica ni aina ya ndege ambaye anajulikana kwakuwa anakula kitu chochote, hana anachochagua. Ni kweli kwamba wajawazito wengi hupata hamu ya kula vitu ambavyo si vyakula walivyozoea kula mara kwa mara wakiwa si wajawazito; wengi wao ni rahisi kuwaelewa kwa sababu hukimbilia mchele, barafu na vinginevyo ambavyo si vitu vibaya kula.

Kwa watoto, hii ni tabia iliyozoelekakwakuwa inawatokea watoto wengi ambao ni kati ya asilimia 25 na 30% ya watoto wote; lakini kwa wanawake wajawazito, inatakiwa iwe kwa kiwango cha chini zaidi.

Nini kinasababisha tabia hii kwa wajawazito?

Sababu ya baadhi ya wanawake kuwa na tabia hii wakati wa ujauzito haijulikani hasa. Kwa sasa hakuna sababu maalumu, lakini kwa mujibu wa Jarida la Chama cha Watu Wanaoishi na Ugonjwa wa Kisukari nchini Marekani, tabia hii yawezekana ikasababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini. Baadhi wanadai kwamba hali hii inaashiria kwamba mwili unajaribu kupata vitamini na madini mengine yanayokosekana kwenye chakula cha kawaida ambacho mtu anakula. Muda wingine tabia hii yawezaikatokana na kuumwa viungo au akili kwa muda mrefu.

Baadhi ya vitu vya ajabu ambavyo wajawazito hupenda kula

Vitu vinavyopendwa zaidi na wajawazito wengi ni udongo, uchafu. Vitu vingine ni njiti za kiberiti zilizochomwa, mawe, mkaa, barafu, dawa ya meno, sabuni na mchanga. Mjamzito anapokula vitu hivi hujisikii raha kana kwamba amekula chakula chenye faida kubwa kwake na kwa mtoto aliye tumboni.

Kuna hatari yoyote kwa mtoto aliye tumboni?

Kula vitu ambavyo si vyakula kimsingi ni jambo linaloweza kusababisha madhara kwa mjamzito mwenyewe na mtoto aliye tumboni. Kula vitu hivi kunaweza kuharibu mfumo wa kawaida wa kunyonya virutubisho kutoka kwenye vyakula na kusababisha mwili wako upungukiwe na madini muhimu unayoyahitaji kwa afya yako na ya ukuaji wa mtoto vilevile. Tabia hii ni hatarishi sana kwakuwa vitu ambavyo si vyakula vinaweza kuwa na viambata ambavyo ni sumu au vyenye vijidudu vinavyoathiri mwili.

Kudhibiti tabia hii

Usihamaki unapojikuta unatamani vitu vya ajabu ajabu wakati wa ujauzito: inatokea sana na si jambo la kushangaza kwako pia. Jambo la muhimu ni kumjulisha muuguzi wako au wahudumu wa kliniki unayohudhuria kujua maendeleo yako ya mtoto tumboni ili akuelimishe na ahakikishe kwamba una uelewa kuhusu hatari zinazoambatana na tabia hiyo.

Baadhi ya mbinu za kutumia kushinda tamaa hizo


  • Mtaarifu mhudumu wako wa afya kwenye kliniki unayohudhuria na muangalie kumbukumbu za ukuaji wa mtoto tumboni pamoja na hali yako ya kiafya
  • Fatilia kiwango chako cha madini ya chuma mwilini pamoja na kiwango cha vitamini na madini mengine unayotakiwa kula
  • Omba ushauri kuhusu kitu gani uwe unakula ili kubadili ili kuepuka vitu vya ajabu (waweza kumung’unya/ kutafuna vitu kama pipi au ‘big g’ isiyo na sukari
  • Mwambie hata rafiki yako mmoja kuhusu hamu hizi na umtake awe anakukataza unapokula vitu vya ajabu
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad