7/23/2020

Joe Biden "Donald Trump Ndiye Mbaguzi wa Kwanza wa Rangi Kuwa Rais wa Marekani"Mgombea wa urais Marekani kwa chama cha Democratic Joe Biden amesema Rais Trump ndiye mbaguzi wa kwanza wa rangi kuwa rais wa Marekani. Kauli hiyo imekanushwa vikali na timu ya kampeni ya Trump.

Biden ambaye alikuwa makamu wa rais katika uongozi wa Rais Barack Obama, Mmarekani mweusi wa kwanza kuwa rais alikuwa anajibu swali la muhudumu mmoja wa afya aliyeuliza kuhusiana na Rais Trump kuviita virusi vya corona, virusi vya China.

Biden amesema katika historia hakuna rais wa Marekani ambaye ashafanya kitu kama hicho. Vita hivi vya maneno kati ya Biden na Trump vinazidi ukizingatia kuwa suala la rangi ni nyeti sana na limekuwa likizungumziwa sana.

Biden na Trump wote ni watu weupe na mmoja kati yao anatarajia kuwa rais wa Marekani baada ya uchaguzi wa Novemba 3.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger