Katika Hali iliyowashangaza Wengi..Watia Nia 55 CCM Wautaka Uongozi Chato Kwa MagufuliKATIKA hali iliyowashangaza wengi, watia nia wapatao 55 wamejitokeza kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili wapitishwe kugombea ubunge Jimbo la Chato.

Jimbo la Chato ndiko nyumbani kwa Rais John  Magufuli ambaye aliliongoza jimbo hilo kwa miaka 20 mfululizo kwa mafanikio makubwa mpaka alipochaguliwa kuwa Rais  mwaka 2015.

Katika vipindi vinne alivyoliongoza jimbo hilo ambalo zamani liliitwa Biharamulo Mashariki, Magufuli alipita bila kupingwa katika vipindi viwili.

Miongoni mwa waliochukua fomu mwaka huu ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani anayetetea nafasi yake.

Taarifa kutoka Chato zinasema Kalemani anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa vijana wasomi wazawa wa Chato ambao wamejitokeza kumpinga.

Uwepo wa watia nia 55 wengine wameutafsiri kuwa ni kutokana na mwamko mkubwa na demokrasia iliyokomaa ndani ya CCM ambapo sasa wanachama wote wana nafasi sawa ya kugombea, tofauti na zamani ambapo walio na fedha ndiyo walikuwa na nafasi.

Pia inadhihirisha kauli ya Magufuli kwamba hana mgombea na kwamba hajatuma mtu kwenda popote kugombea bali kura za wajumbe ndizo zitakazoamua.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments