Kauli ya Kubenea baada ya kuhamia ACT Wazalendo akitokea CHADEMA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA Saed Kubenea, amesema kuwa maamuzi ya yeye kujiunga rasmi na chama cha ACT Wazalendo yalikuwa ni magumu, kwa kuwa hicho ndiyo chama chake cha pili kujiunga tangu aanze siasa na kudai kuwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam upinzani una nguvu kubwa.



Saed Kubenea.


Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 18, 2020, mara baada ya kujiunga rasmi na chama cha ACT Wazalendo, na kupokelewa na kukabidhiwa kadi ya uanachama na Mwenyekiti wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.


“Kwa kweli maamuzi haya yalikuwa ni magumu sana kwa sababu katika maisha yangu, hiki ndiyo chama cha pili kujiunga lakini nilifika mahali nikasema, kama Maalim Seif alinzisha CUF kwa jasho na damu akaondoka, baada ya kutoridhika na hali iliyokuwa ikiendelea sembuse mimi, nikajifunza kwamba ni lazima safari hii ya mabadiliko iendelee”, amesema Kubenea.


Hivi karibu Kubenea wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, alisema kuwa miongoni mwa sababu zilizopelekea yeye kutogombea tena Ubunge wa jimbo la Ubungo kupitia CHADEMA ni pamoja na uwepo wa migawanyiko ndani ya chama na kusakamwa kwake kusikokuwa na sababu ndani ya chama hicho.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kubenea, uko ni bomu.
    naona urudishe hiyo kadi. Chama Dili kwa sasa baada ya CCM ni NCCR.
    Usichelewe, hukunishauri kabla.

    Hawa Dogo wote, si jitto wala mtowe
    wote wanamiliki saccozi kama mali binafsi.. Usihadaike na matokea ya MAALIM kumfanyia inda Plofesa na hatimaye kumuachia chama.unajua tatizo
    uliza upate jibu. Si jingine ni Ruzuku
    na hapo ndicho kitacho tokea.

    Membe oyee.. Mbatia Safiii..!!

    ReplyDelete

Top Post Ad