7/24/2020

Kenyatta Atangaza Siku 3 Kumwomboleza Mkapa


RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kwa nchi hiyo kuanzia Jumatatu ijayo hadi Jumatano, kutokana na kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Julai 24, 2020.

Kenyatta amesema bendera ya Kenya na Jumuiya ya Afrika Mashariki zitapepea nusu mlingoti kuanzia Julai 27, 2020 hadi Julai 29, 2020 ikiwa ni sehemu ya kuomboleza kifo hicho na kumuenzi kiongozi huyo wa Tanzania.

“Nawapa pole Watanzania wote na familia ya Mkapa kwa kuondokewa na mpendwa wenu, Mkapa alikuwa kiongozi bora aliyesimama kidete kuiungansha Afrika Mashariki,” amesema Kenyatta.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger