7/31/2020

Kimenuka...Balozi wa China Amedai Marekani Inataka Kuanzisha VITA na China


Balozi wa China nchini Uingereza amesema leo kuwa Marekani inajaribu kuanzisha vita baridi mpya na taifa hilo la kikomunisti kwa sababu inatafuta kisingizio kuelekea uchaguzi wa rais mwezi Novemba.

Balozi huyo Liu Xiaoming, amesema siyo nchi yake iliyogeuka mbabe bali ni upande wa pili wa bahari ya Pacific unaotaka kuanzisha vita mpya baridi dhidi ya China, na hivyo wanalaazimika kujibu hilo.

Balozi huyo aliezungumza na waandishi habari, ameongeza kuwa China haina maslahi yoyote katika vita baridi, na wala haitaki vita vyovyote.

Amesema wameona kila kinachoendelea nchini Marekani, wakitaka kuitumia China kama kisingizio na kuilaumu kwa matatizo yao, na kwamba wanajua hii ni kwa sababu mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger