Kinda mwenye uwezo wa ‘AJABU’ kutua Man United, miaka 16 magoli 600


Kinda, Charlie McNeill wa miaka 16 anayefananishwa na Paul Scholes anatarajiwa kutua Manchester United baada kugoma kuingia kandarasi na Manchester City.

Inawezekana isieleweke kwa haraka lakini Manchester United inanafasi kubwa ya kumsajili kinda huyo ambaye amenuia kuondoka ndani ya Manchester City.

Katika taarifa iliyotolewa leo siku ya Ijumaa kupitia mahojiano na Sportsmail, Man United wanayonafasi kubwa ya kumsaini mshambuliaji huyo wa miaka 16, Charlie McNeill ambaye mpaka sasa ameshafunga jumla ya magoli 600 katika mashindano  mbalimbali ya vijana.

Nyota huyo wa Kimataifa wa England amekataa kuingia mkataba na Man City wiki sita zilizopita katika dimba la Etihad Stadium na United wanahitaji kumnyakuwa baada kuondoka kwao miaka sita iliyopita.

Kwakuwa McNeill hajafikisha hata umri wa miaka 17 anafikisha mwezi Septemba, klabu hizo mbili zitalazimika kusubiri kwanza au kuingia makubaliano ya pande zote mbili.

McNeill scored an astonishing 110 goals in 72 matches during his time with Man City under-15s

Bahati mbaya McNeill ni mnazo mkubwa wa United na alikuwa na mafanikio makubwa katika kucheka na nyavu alipokuwa huko na akayaendeleza mafanikio hayo akiwa City.

Akiwa na miaka 15, amefanikiwa kufunga magoli 110 na kutoa ‘assists’ 38 kwenye mechi zake 72 tu alizocheza akiwa ndani ya Man City.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments