7/28/2020

Kisa cha Wanafunzi Wawili Waliozikwa Hai Kisumu


Wanne hao walijipata msibani walipokuwa wakichimba mchanga

Wawili walinusurika kifo kwa majeraha mabaya huku wawili wakipoteza maisha yao

Hali ya huzuni na masikitiko imegubika kijiji cha Angola, katika kaunti ndogo ya Kisumu baada ya wanafunzi wawili kuripotiwa kuzikwa hai walipokuwa wakivuna mchanga.

Mgodi huo uliwafunika ghafla wanafunzi wanne Jumatatu, Julai 27 walipokuwa wakishirikiana katika kuvuna mchanga wawili wakinusurika na wenzao kuangamia muda mfupi baadaye.

Kulingana na  Maurice Onyango ambaye ni mkazi wa eneo hilo, wanafunzi wote wanne walitolewa katika shimo hilo na kufikishwa katika zahanati ya Angola ambako wawili walithibitishwa kufariki.

Miili ya wawili hao waliofariki ilisafirishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha St. Elizabeth na Jaramogi Oginga Odinga mtawalia.Wawili wengine walionusurika wanaendelea kupokea matibabu hali yao ikizidi kuimarika. Picha: Hisani

Mwakilishi wadi Steve Owiti alituma salamu za rambirambi kwa jamaa na marafiki ya wanafunzi hao na kuwaomba wenyeji kutafuta riziki kwa njia mbadala na wala si kuhatarisha maisha katika migodo ya mchanga.

‘’ Nimehuzunika mno. Inahofisha sana. Lakini inabdi tutafute kazi mbadala, badala ya kuhatarisha maisha yetu,’’ Owiti alisema.

Inadaiwa kuwa licha ya watu kupoteza maisha yao katika migodi hiyo, wakazi wa eneo hilo wanasisitiza kuwa hiyo ndiyo ajira yao na ni vigumu kuiacha.

Wanafunzi hao waliopteza maisha walikuwa katika kidato cha tatu.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger