Kufuru Mondi Anunua Nyumba 10 Tabata-Segerea, Dar
ALIYENA-CHOanao-ngezewa! Msemo huo umeji-dhihirisha kwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kufanya kufuru nyingine ya kununua nyumba 10 kwa pamoja huko Tabata-Segerea jijini Dar es Salaam.

Awali, zilisambaa tetesi kuwa staa huyo amenunua nyumba hizo kama ‘apartment’ kwa ajili ya kupangisha ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu atangaze kununua nyumba nyingine huko Kigamboni.“Ni kama mtaa mzima kanunua, maana nyumba zote hizo zipo ndani ya uzio mmoja,” alisema jirani aliyejitambulisha kwa jina la Aika.


AMANI MZIGONI

Ili kujua ukweli kuhusiana na suala hilo, Amani lilifunga safari moja kwa moja mpaka maeneo hayo na kufanikiwa kujionea nyumba hizo ambazo zilikuwa zikifanyiwa ukarabati.

MAJIRANI WAZUNGUMZA


Kabla ya kuzama ndani, gazeti hili lilizungumza na baadhi ya majirani wa mtaa huo ambapo kila mmoja alifunguka kwa namna yake.


“Ni kweli Mondi kanunua huu mjengo, hata hapa juzikati alikuja kwa ajili ya kuziangalia,’’ alisema kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mzenji.Mbali na Mzenji, jirani mwingine ambaye yeye hakuwa tayari jina lake kuandikwa gazetini, alisema kuwa nyumba hiyo ilikuwa ikimilikiwa na mfanyabiashara mmoja hivi (jina hakulitaja) ambapo baadaye alipata tatizo lililopelekea kuiuza.

“Ni kweli jamaa (Mondi) kanunua hii nyumba, na msione hivi, humo ndani zipo nyingi na inabeba wapangaji kibao tu, ila inasemekana aliyekuwa mmiliki alipata matatizo hivyo akaamua kumuuzia Mondi kama Milioni 250,” alisema.

MAFUNDI WAFUNGUKA


Amani lilipomaliza kuzungumza na majirani hao, lilizama ndani ili kujionea ambapo lilikutana na mafundi wawili waliokuwa wanaendelea na ujenzi na kupiga nao stori mbili tatu

Japo mwanzo walikuwa wagumu kuzungumza, lakini baada ya kuwashawishi sana, walikubali na kutoa ushirikiano ambapo mmoja wao anayejulikana kwa jina la Fundi Hamisi alikiri kuwa ni kweli Mondi amenunua nyumba hizo na ziko katika hatua ya matengenezo.

“Hizi nyumba ni za Mondi na hapa unavyoona tupo kwa ajili ya kuzifanyia marekebisho, hivyo baada ya miezi miwili au mitatu hivi, zitakuwa tayari zimeshakamilika kwa sababu mama yake Sanura Kassim ‘Mama Dangote’ huwa anakuja mara kwa mara kuangalia maendeleo,” alisema.Alipotafutwa Mondi ili aweze kuzungumzia zaidi suala hilo, simu yake iliita muda mrefu bila kupokelewa.

TUJIKUMBUSHE

Hii siyo mara ya kwanza msanii huyo kununua nyumba, miezi michache iliyopita alitangaza kununua hoteli maeneo ya Mikocheni, pia hakuishia hapo, akasema kuwa ameanza ujenzi wa mjengo wake wa kisasa uliopo Kigamboni jijini Dar.

Hata juzi kwenye sherehe iliyoandaliwa na Lebo hiyo baada ya kutoka kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika mjini Dodoma, msanii huyo alisikika akisema kwamba, amenunua nyumba mbili huko Dodoma, hivyo kama ni kweli atakuwa ni miongoni mwa wasanii wanaotumia pesa zao vizuri kwa ajili ya kuwekeza kwenye ardhi. Waandishi: Memorise Richard na Khadija Bakari.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments