Lampard Ataja Faida ya Chelsea Kufuzu UEFA
KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amefurahia kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao akisisitiza hiyo itasaidia kuwavutia wachezaji wapya kwa lengo la kuimarisha kikosi chao.


 


Kiungo huyo wa zamani wa Chelsea, amefanikiwa kuipeleka Chelsea kwenye michuano hiyo mikubwa barani Ulaya katika msimu wake wa kwanza tu akiinoa timu hiyo baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Wolves, Jumapili.
“Tunajua kwamba uchumi wa Ligi ya Mabingwa ni mkubwa, tunajua hilo,” alisema Lampard.


“Tunajua hadhi ya ligi hiyo, wachezaji wakubwa wanataka kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lakini kama tunataka kuboresha kikosi chetu kwenye baadhi ya nafasi, hilo litasaidia…tutajaribu kujiboresha kwa vyovyote tuwezavyo.”
Chelsea imebakiza mechi mbili kumaliza msimu, dhidi ya Arsenal kwenye fainali ya FA na dhidi ya Bayern katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern kujaribu kupindua matokeo ya kufungwa 3-0 nyumbani.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments