Madagascar Yaomba Msaada Kukabiliana na Corona

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wizara ya afya nchini Madagascar imetuma ombi la msaada wa dharura kwa mashirika na taasisi za Afya huku wagonjwa wa corona wakiongezeka. Wizara ya Afya imesema kwamba ugonjwa huo katika wiki za hivi karibuni umesambaa kwa kiwango cha juu nchini Madagascar huku maeneo kadhaa yakirekodi milipuko hususani mji mkuu wa Antananrivo, kulingana na mtandao wa Actu Orange. 

Kumekuwa na ripoti kwamba hospitali za umma nchini Madagascar zimejaa na zimekuwa zikiwalaza wagonjwa walio katika hali mbaya zaidi. Taifa hilo kwa sasa lina takriban wagonjwa 7000 wa Covid-19. Rais Andry Rajaolina mapema mwezi huu aliweka masharti ya kutotoka nje katika mji mkuu wa Antananarivo kufuatia kuongezeka kwa maradhi hayo. 

Mnamo mwezi Aprili, alizindua dawa ya mitishamba ya maradhi ya Covid-19 ambayo ilisambazwa nchini humo. Mizigo kadhaa ya dawa hiyo ya Covid Organic pia ilitumwa kwa makumi ya mataifa barani Afrika. 

Hatahivyo uwezo wa kinywaji hicho umepuuziliwa mbali na wataalam wa Afya nchin NIgeria na DR Congo mataifa ambayo yalifanyia majaribio dawa hiyo. 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad