Makubwa! Msichana Apachikwa Mimba na Babake Mzazi wa KumzaaFamilia moja huko  Kajiado imejipata katika  njia panda kuhusu hatua inayofaa kuchukuliwa baada ya msichana  kutungwa mimba anayodai ni ya babake wa kumzaa.

Msichana huyo wa shule ya upili  anadaiwa kupachikwa mimba na mzazi wake mwezi Machi  lakini babake anakanusha kwamba ndiye aliyehusika na tukio hilo huku polisi wakianzisha uchunguzi. Watu wa familia wameshindwa watachukua hatua gani kati ya kuitoa mimba ya msichana huyo au kungoja hadi ajifungue ili kufanya vipimo vya DNA ili kumjua baba  ya mtoto wake.

 Mischana anadai kwamba babake amekuwa akimdhulumu kimapenzi kwa muda mrefu lakini  hakuwahi kuripoti tukio hilo. Katika hatua ya kujikaanga, babake amekiri kwamba ni kweli alikuwa akifanya mapenzi na binti yake lakini siye aliyemtunga mimba kwani alikuwa akitumia  mpira wa kondomu.

Kesi hiyo ipo kortini  na  majina ya wahusika hayawezi kutolewa bila kukiuka haki zao lakini kisa hicho kimewashangaza watu wengi katika sehemu husika. Mwezi uliopita, mamake msichana aliwasilisha ombi kwa jaji ili wawaruhusu madaktari waitoe mimba hiyo kwa sababu  itakuwa laana kwa binti yake kumzaa mtoto ambaye hajui atamuitaje  babake-mjukuu wake ama babake na pia kuna tishio la wazee wa jamii kuifukuza familia hiyo kutoka ukoo wao.

‘Kuna  mengi kuhusu mila na desturi na alichofanya mzee wa boma hilo iwapo ndiye aliyempachika mimba bintiye basi kutakuwa na matatizo’ amesema mzee mmoja wa kijiji.

 Jamaa za mwanamme huyo hata hivyo wameibuka na madai mengine wakimtetea kwamba binti huyo sio wake kwa sababu mamake alikuja naye akiwa mdogo na yeye amekuwa tu babake mlezi. Hatua hiyo hata hivyo huenda  isimpe  afueni hata endapo itathibitishwa kwamba msichana huyo  sio mtoto wake kwa sababu yungali ni mwanafunzi na sasa hatua ya kupachikwa mimba itavuruga masomo yake.

Mahakama haijatoa uamuzi kuhusu ombi la mama msichana kuitaka mimba hiyo itolewe lakini kwa sasa mwanamme mwenye nyumba amepewa agizo la kutokaribia familia yake hadi suala hilo litatuliwe.

 ‘Kuna uwezekano kwamba licha ya baba kuwa alikuwa akifanya mapenzi na msichana huyo siye aliyempa mimba lakini bado ana kosa la kushiriki mapenzi na bintiye hata iwapo yeye sio babake mzazi’ amesema jamaa mmoja ambaye ni jirani yao.

Polisi wanasema mengi yataamuliwa na uchunguzi wa madaktari na mahakama kwa sababu mambo mengi katika tukio hilo I madai ya upande mmoja dhidi ya pingamizi kwa kutoka upande wa pili.

That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments