7/24/2020

Mama Nandy Afunguka Ndoa Ya Mwanae “Simkubali Sana Billnass”

Mama wa mwanamuziki Nandy ameshindwa kuzungumzia juu ya ndoa ya mtoto wake na msanii mwenzi Billnas ambaye alimvesha pete ya uchumba hivi karibuni kabla ya kufanya utambulisho rasmi kwao.

Akizungumza na wanahabari wakati wa shughuli ya kufunguliwa kwa duka la kuuza magauni ya harusi jijini Dar es salaam Mama Nandy alishindwa kueleza iwapo anampenda mkwe wake huyo mtarajiwa au la.

“”Mambo ya ndoa ni mipango ya Mungu, wengi wanatamani kumuona Nandy anaolewa ila Mungu akipenda harusi itakuwepo, kama mzazi bado, Mkwe siwezi sema namkubali au simkubali kwa sababu Nandy ndio anaolewa sio mimi, yeye ndio kamkubali, yeyote atakayetuletea hata kama ni kichaa kwetu sawa” amesema Mama Nandy.

Nandy alifanya shuguli ndogo ya kufungua duka lake la kuuza vifaa kwa harusi kwa kinadada ambalo limeanza kufanya kazi leo baada ya kujihusha muda mrefu na shughuli za ushonaji wa nguo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger