Manchester United na Chelsea zafuzu kucheza Champions League


Manchester United na Chelsea zimefuzu kucheza Champions League baada ya Manchester United kuipiga kikumbo klabu ya Leicester katika siku ya mwisho ya mechi za ligu kuu ya Uingereza, Premier jana Jumapili.

Manchester United ilipiga Leicester bao mbili kwa nunge na kufanikiwa kumaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu huku ushindi wa Chelsea wa mabao 2-0 dhidi ya Wolverhampton uliiwezesha timu hiyo kuchukua nafasi ya nne na kufuzu kucheza Champions League.

Leicester ambayo ilishikilia nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kwenye kipindi chote cha msimu, imeangukia pua kwa kumaliza nafasi ya tano na hivyo kujinyakulia tiketi ya kucheza ligi ya Ulaya ikijiunga pamoja na Tottenham Hotspurs.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments